SERIKALI imeshauriwa kuweka adhabu kali ili kudhibiti wanaotumia mitandao ya kijamii vibaya ikiwamo kutoa habari zenye nia ya kuchochoe machafuko na za uongo.
Ushauri huo umetolewa Leo Oktoba 26 Jijini Dar es Salaam katika majadiliano ya pamoja kati ya waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo vya habari mitandaoni. Akifungua pazia la kuchangia hoja katika mjadala huo, Mpigapicha na Mwandishi wa Habari Mkongwe, Muhidini Michuzi alisema kinachoendelea mitandaoni kimetokana na wananchi kuaminishwa propaganda mbaya.
"Ni muhimu kutoa maoni yenye heshima ili kuepuka kutweza utu wa mwingine kwa kuwa machafuko sio sehemu ya desturi ya watanzania" amesema Michuzi Mchangiaji mwingine, Imani Luvanga ambaye pia ni mwandishi wa Habari, ameshauri kuwe na elimu ya matumizi sashimi ya mitandao ya kijamii na kwamba itasaidia watumiaji kuwa na uelewa.
"Mtandao ukifungwa watu wengi wanapoteza fedha, kila mmoja anahitaji kuwa 'free' (huru) kwa kufanya kitu ambacho hakiwezi kuvuruga maisha ya wengine. "Ikitokea Mwandishi wa Habari umesambaza taarifa za uongo ni muhimu kutoka na kuomba radhi kwa sababu kwa kufanya hivyo itasaidia wasomajj kuendelea kukuamini" amesema Imani
Aidha ameongeza ipo haja ya watawala kuheshimu wanaotoa maoni na kuyafanyia kazi ili kuepuka kuifunga mitandao kwa kuwa kufanya hivyo kinafanya watu wapoteze fedha nyingi. Amesisitiza njia ya kutatua tatizo sio kulikimbia bali ni kuangalia wapi pamekosewa na kutafuta upya njia ya kujenga taifa ikiwamo serikali kuchukua hatua za haraka.
"Kijana inapaswa ujue kwanini upo mtandaoni unataka nini na unataka kufanya nini hii itatusaidia kuwafanya vijana wasiposti vitu vya hovyo" amesema Mwandishi wa Habari mwingine, Juma Hassan ameshauri serikali iendelee kutoa elimu ya namna sahihi ya vijana na waandishi wa habari kutumia mitandao ya kijamii.
Amesema kwa kufanya hivyo itasaidia kupunguza wanaosambaza habari za upotoshaji ambazo mara nyingi huleta taharuki katika jamii. "Vijana tusiammae katika kutengeneza maudhui yenye kulenga kuhamasisha utulivu na amani" amesema
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED