Mgombea urais kupitia Chama cha NLD, Doyo Hassan Doyo, amesema chama chake kimejipanga kwa dhati kuwakomboa vijana wa Kitanzania kupitia elimu bora yenye kuzingatia vitendo kama suluhisho la changamoto za ajira na utegemezi.
Akizungumza jana katika mikutano ya kampeni mkoani Morogoro, Doyo amesema mfumo wa sasa wa elimu umekuwa ukizalisha wahitimu wasiokuwa na uwezo wa kujitegemea au kubuni miradi ya maendeleo, jambo linalochangia ukosefu wa ajira kwa vijana wengi.
“Tunataka elimu inayomwandaa kijana kujiamini, kubuni miradi na kujiajiri. Elimu ya kukariri bila ujuzi wa vitendo imeshindwa kuwasaidia vijana wetu,” amesema Doyo.
Ameongeza kuwa, kupitia Ilani ya Uchaguzi ya NLD 2025–2030, chama hicho kitaleta mageuzi makubwa katika mfumo wa elimu nchini kwa kuhakikisha mitaala inazingatia mahitaji halisi ya soko la ajira na ujuzi wa kazi.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED