Bodaboda, Machinga kutofanya kazi Desemba 9

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 09:06 AM Nov 24 2025
Bodaboda, Machinga kutofanya kazi Desemba 9

Maofisa wasafirishaji ' bodaboda na wafanyabiashara' machinga' wa Mkoa wa Dar es Salaam wamesema Desemba 9,2025 hawatafungua shughuli zao baada ya kuwepo kwa taarifa za maandamano yanayoratibiwa kinyume na utaratibu.

Wamewataka wenzao wanaojishughulisha na shughuli hizo kubaki kwenye majumba yao, huki wakiwaonya watakaoidia na kukumbwa na matatizo kuwa hawatahusika nao.

Wameeleza hayo wakati wa kikao chao na pamoja wakuu wa wilaya mbalimbali akiwemo wa Ilala, Edward Mpogolo na Julius Mtatiro wa Shinyanga.


"Hatufungua maeneo yetu ya biashara, maana wanaweza kusema machinga walikuwa wanaandamana, tutakwenda kuzungumza na wenzetu, kupitia kusanyiko hili.Tutafunga biashara ili yule atakayekwenda Kariakoo kwa kisingizio cha machinga atakumbana na mkono wa dola, sisi tunataka amani na utulivu," wamesema.