Kibatala aibua mapya sakata la Polepole, kesi yahairishwa mpaka Oktoba 15

By Imani Nathaniel , Nipashe
Published at 06:08 PM Oct 09 2025
Kibatala aibua mapya sakata la Polepole, kesi yahairishwa mpaka Oktoba 15

Mawakili Peter Kibatala na Dickson Matata wamefungua shauri Mahakamani wakizitaka mamlaka zinazohusika na ulinzi na usalama wa raia na mali zao kuhakikisha zinamtambua alipo au kumfikisha Mahakamani aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi na Cuba, Humphrey Polepole, ambaye anadaiwa kutoweka tangu Novemba 6, mwaka huu.