Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, amesema uongozi wa miaka ya sasa umekuwa tofauti, kwa kuwa walio wengi wamejilimbikizia mali, kuliko wanaowaongoza.
“Leo unamkuta kiongozi ana mali nyingi. Unaweza kumuuliza umezipata wapi, maana sisi tumekuchagua wewe utuongoze sisi kwenye kuzipata, sio wewe uongoze kwenye kupata.
“Uongozi wa kuwaongoza watu ni mgumu, Mwalimu alituambia kuwatumia watu kuna wakati moyo unaumia, unaona watu wanashida…ukiishi kwa ajili ya watu utaishi milele.
"Mwalimu Nyerere kafa maskini…aliishi kwa ajili ya watu, mtu anaweza kuwa si mkatoliki, mlokole si muislamu ila anavyoishi anaishi kwa ajili ya watu,” amesema.
Amesema dunia ya sasa imejaa watu wenye nguvu, unaweza kupewa nafasi na Mungu uwatumikie watu lakini ukawaumiza watu: “Angalia kina Kwame Nkrumaha, Thomas Sankara alitoa maisha yake kwa ajili ya watu, alitumia baskeli”.
Askofu Gwajima ameyasema hayo leo, Januari 25, 2026 kwenye ibada katika kanisa hilo, Dar es Salaam, na kwamba zipo faida za kumtumikia Mungu, pamoja na jamii kwa upendo.
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED