Mabaharia wazoefu waliodumu katika shughuli za baharini kwa zaidi ya miaka 40, wamewahamasisha watanzania kuipenda, kuijali na kuithamini nchi yao kwa kutembelea vivutio vya utalii wa ndani na kujivunia uwekezaji unaoendelea nchini.
Akizungumza katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mabaharia Wazoefu Tanzania, Juma Simba Ghadafi, amesema utalii wa ndani una mchango mkubwa katika kukuza uchumi na ajira kwa vijana.
Amesema filamu ya Royal Tour, imeiweka Tanzania kwenye ramani ya dunia na imeongeza hamasa ya watanzania wenyewe kutembelea hifadhi na vivutio vyao na ndio maana na wao wamesukumwa kuunga mkono jitihada zilizofanywa na Rais kuutangaza utalii.
Amesema filamu ya Royal Tour imeonesha uzuri wa nchi na kuwafanya watanzania wajivunie rasilimali zao, huku utalii wa ndani ukiwa nguzo ya mshikamano na maendeleo.
Mahabaria hao wenye umri kati ya miaka 62 hadi zaidi ya 80, ambao kupitia umoja walioanzisha wamekuwa wakisaidiana shughuli na mahitaji mbalimbali, ikiwamo kuwakatia bima wahitaji.
Mmoja wa mabaharia Shahibu Ngota, amesema usafiri wa treni ya SGR umeleta faraja na kasi kwa wasafiri na kwamba safari yao kwa treni ilikuwa salama, ya haraka na yenye mandhari mazuri, jambo lililoongeza furaha ya kutembelea Mikumi.
Shahibu Ngota, amesema SGR imepunguza muda wa safari na gharama na imefungua fursa za kibiashara na utalii katika mikoa mbalimbali.
Katibu wa Umoja huo, Danny Masele na Baharia Mohamed Jagga, wamefurahia ziara yao kwa kujionea vivutio mbalimbali wakiwemo wanyamapori katika hifadhi ya Mikumi, tamaduni, mila na desturi eneo la Masai Boma Mikumi na kuona ipo haja watanzania wengi wakapenda vya kwao.
"Unaweza kuta mtu ameishi miaka yake yote hajui Tanzania ina vivutio gani, wanatoka watu kutoka mbali wanatuacha hapa hapa,” amesema Masele.
0000
Picha
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED