Jumuiya ya Wadau wa Parachichi Tanzania (ASTA), kupitia Mwenyekiti wake mpya, imesema itahakikisha inasimamia kikamilifu mchakato wa ujenzi wa kiwanda kipya cha kuchakata mafuta yatokanayo na zao hilo, hatua itakayosaidia kuongeza thamani.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wadau wa Parachichi Tanzania (ASTA), Emmanuel Kisinda, wakati wa mkutano wa jumuiya hiyo uliofanyika Halmashauri ya Mji Njombe.
Kisinda amesema kuwa jumuiya hiyo imelenga kuhakikisha kiwanda cha kuchakata parachichi kinajengwa ndani ya mwaka 2026.
Aidha, amebainisha kuwa ASTA itaendelea kuhamasisha ongezeko la wanachama, kwa sasa jumuiya hiyo ina wanachama wasiopungua 3,000 wakiwamo wakulima, ili kuongeza uelewa kuhusu ASTA na majukumu yake.
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED