slot gacor
slot gacor
slot gacor
Dar yapanda miti kumbukizi ‘birthday’ ya Samia | Nipashe

Dar yapanda miti kumbukizi ‘birthday’ ya Samia

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 07:39 PM Jan 27 2026
Dar yapanda miti kumbukizi  ‘birthday’ ya Samia
Picha: Mpigapicha Wetu
Dar yapanda miti kumbukizi ‘birthday’ ya Samia

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewaongoza wakazi wa Manispaa ya Temeke kupanda miti 200 katika Shule ya Msingi Goroka A, Kata ya Toangoma, kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Zoezi hilo lilifanyika Januari 27, 2026, likiambatana na kukata keki ya kumtakia Rais Samia heri na afya njema, kama ishara ya kuunga mkono kampeni ya kupanda miti kusherehekea siku hiyo muhimu.

Chalamila amewasihi wakazi wa Dar es Salaam na wadau wa mazingira kuunga mkono kampeni hiyo ili kusaidia juhudi za utunzaji wa mazingira.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Great Leaders, Dk. Deborah Elisha, amesema wanahamasisha upandaji miti kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kuwachagua watoto kuanzia shule kuwarithisha tabia ya kutunza mazingira.

Ameongeza kuwa Watanzania wanapaswa kumuombea Rais Samia na viongozi wengine ili waweze kutimiza majukumu yao ipasavyo.

Mhifadhi Mkuu wa TFS, Manispaa ya Temeke, Selewin Regie, amesema wakala huo unakusudia kupanda miti milioni moja mwaka huu na kuwakaribisha wananchi kupata miti ya matunda, dawa na kivuli bure.

Mkuu wa Shule Goroka A, Steven Kailembo, ameahidi kushirikiana na wadau kuondoa jangwa shuleni hapo na kwamba upandaji miti ni ajenda yao ya kudumu. Alisema tangu shule ilipoanzishwa mwaka 2022 ilikuwa jangwa lakini kwa kushirikiana na wadau, wameweza kupanda miti iliyojaliwa na wanafunzi.

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda, Meya wa Manispaa Uzairu Athman, Naibu Meya, viongozi wa CCM na wadau wa mazingira.