slot gacor
slot gacor
slot gacor
CCM Moro kujitathimini kwa vitendo utekelezaji wa Ilani yake | Nipashe

CCM Moro kujitathimini kwa vitendo utekelezaji wa Ilani yake

By Christina Haule , Nipashe
Published at 06:13 PM Jan 30 2026
Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro Nuru Ngereja.

Chama cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Morogoro kimejipanga kujitathimini kwa kufanya shughuli mbalimbali, ikiwemo kukagua utekelezaji wa Ilani ya chama pamoja na kutembelea miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Mvomero.

Hatua hiyo ni kuelekea maadhimisho ya miaka 49 ya kuzaliwa CCM Januari 31, mwaka huu

Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro Nuru Ngereja, amesema kuanza maadhimisho ya sherehe hizo yatafanyika Turiani Wilani Mvomero, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro Mhandisi Joseph Masunga,wakati  kilele kikifanyika Februari 5 katika Halmashari ya Wilaya ya Mlimba na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa UVCCM taifa Mohamed Kawaida.

Ngereja amesema lengo la maadhimisho hayo ni kuhakikisha chama kinajitathmini kwa vitendo utekelezaji wa Ilani yake,  kujionea maendeleo yanayotekelezwa kwa manufaa ya wananchi, badala ya kufanya sherehe za kawaida.

Amesema miongoni mwa miradi itakayokaguliwa ni Hospitali ya Wilaya ya Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, pamoja na miradi mingine ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya mkoa huo.

“Maadhimisho haya ni fursa ya chama kujipima, kuona utekelezaji wa Ilani na kusikiliza changamoto za wananchi ili kuzitafutia ufumbuzi,”.

Katibu huyo wa Mkoa amezungumzia siku 100 za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, akisema kuwa zimeanza kuleta matokeo chanya ndani ya Mkoa wa Morogoro, hususani katika sekta ya afya kupitia utekelezaji wa mpango wa Bima ya Afya kwa Wote.

Ngereja amesema serikali inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya mkoa huo, ikiwemo miradi ya maji, ujenzi na ukarabati wa barabara pamoja na ujenzi wa vituo vya afya, miradi ambayo inalenga kuboresha huduma za kijamii na kuinua maisha ya wananchi.