slot gacor
slot gacor
slot gacor
CBWSO zapewa pikipiki kuboresha huduma za maji kwa wananchi | Nipashe

CBWSO zapewa pikipiki kuboresha huduma za maji kwa wananchi

By Marco Maduhu , Nipashe
Published at 07:02 PM Jan 22 2026
CBWSO zapewa pikipiki kuboresha huduma za maji kwa wananchi
PICHA: MARCO MADUHU
CBWSO zapewa pikipiki kuboresha huduma za maji kwa wananchi

Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira (RUWASA) Mkoa wa Shinyanga, umekabidhi pikipiki tano kwa watoa huduma ya maji ngazi ya jamii (CBWSO), kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi.

Makabidhiano ya pikipiki hizo yamefanyika leo, katika Ofisi za RUWASA Mkoa wa Shinyanga.  Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Kaimu Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga, John Singolile, amewataka viongozi wa CBWSO kuzitumia pikipiki hizo kwa madhumuni yaliyokusudiwa, ili kuongeza ufanisi wa utendaji wao na kutatua changamoto za huduma ya maji kwa wakati.

Amesema pikipiki hizo lengo lake ni kuwawezesha watoa huduma hao kufika kwa haraka katika maeneo yenye changamoto za maji, ikiwamo kufanya matengenezo ya miundombinu na kushughulikia malalamiko ya wananchi kwa wakati.

1


“Lengo la pikipiki hizi ni kuboresha utendaji wenu kazi, na kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama kwa wakati, na mzitumie kwa madhumuni yaliyokusudiwa ili ziwe na tija,” amesema Singolile.

Kwa upande wake, Ofisa Manunuzi wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga, Edmond Kanonika, amesema pikipiki hizo zenye thamani ya Sh. milioni 14.6 zimekabidhiwa kwa CBWSO nne, ambapo CBWSO ya Songambele imepewa pikipiki mbili, huku CBWSO za Mahembe, Solwa na Bulyanhuru zikipewa pikipiki moja moja.

Monica Francis, mmoja wa viongozi wa CBWSO amesema pikipiki hizo zitawawezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi, na kuboresha utoaji wa huduma ya maji kwa wananchi, ikilinganishwa na hapo awali, ambapo walikuwa wakitumia usafiri wa baiskeli.