slot gacor
slot gacor
slot gacor
Chalamila awataka wafanyabiashara Temeke kujipanga | Nipashe

Chalamila awataka wafanyabiashara Temeke kujipanga

By Imani Nathaniel , Nipashe
Published at 04:17 PM Jan 27 2026
Chalamila awataka wafanyabiashara Temeke kujipanga
Picha: Iman Nathaniel
Chalamila awataka wafanyabiashara Temeke kujipanga

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewaomba wafanyabiashara wa Temeke kujipanga vyema ili kujikwamua kiuchumi na kuingia kikamilifu katika uchumi wa soko.

Chalamila ametoa kauli hiyo wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya mikopo ya asilimia 10 yenye thamani ya Sh. bilioni 7.5 kwa vikundi 237 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, akisisitiza kuwa uchumi hustawi katika mazingira ya amani na mshikamano.

Amehimiza wananchi wa Temeke kuzitumia kikamilifu fursa za kiuchumi na mikopo hiyo ili kukuza vipato na kupunguza umasikini, huku akiwapongeza kwa matumizi sahihi ya mikopo na kuwataka kurejesha kwa wakati ili wengine wanufaike.

Aidha, ameeleza kuwa mikopo hiyo ni halali na hutolewa kwa mujibu wa sheria, na kumuagiza Mkuu wa Wilaya ya Temeke kuhakikisha elimu ya ujasiriamali na fursa za ajira zinatolewa kwa vijana na wanawake ili kupunguza changamoto ya ajira.