slot gacor
slot gacor
slot gacor
CRDB yazindua ofisi ya Dubai, kuunganisha mitaji ya kimataifa | Nipashe

CRDB yazindua ofisi ya Dubai, kuunganisha mitaji ya kimataifa

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 06:14 PM Jan 21 2026
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.
Picha:Mpigapicha Wetu
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.

Benki ya CRDB imezindua rasmi Ofisi yake ya Uwakilishi ya Dubai katika hafla iliyofanyika jana Dubai katika hoteli mashuhuri ya Intercontinetal, ikiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Balozi Kombo ameipongeza Benki ya CRDB kwa hatua hiyo muhimu akisema inaiweka Tanzania pamoja na ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, katika uchumi wa pamoja unaokaribia dola za Marekani bilioni 800, moja kwa moja katika mfumo wa mitaji ya kimataifa, ikifanya Benki hiyokazi kama daraja kati ya fursa za kikanda na masoko ya fedha ya kimataifa.

Akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema ofisi hiyo ya Dubai itatumika kama jukwaa la kimkakati la kuwezesha biashara, wawekezaji na pamoja na kuchochea upatikanaji wa mitaji ya kimataifa kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo Tanzania na katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.

Hafla ya uzinduzi ilihudhuriwa na watu zaidi ya 700 wakiwamo viongozi wakuu wa Serikali, wawekezaji wa kimataifa, taasisi za fedha za kimataifa na washirika wa maendeleo. Ushiriki huu unaashiria kuongezeka kwa imani ya kimataifa kwa Benki ya CRDB kama daraja linaloaminika kati ya Afrika na masoko ya kimataifa.