slot gacor
slot gacor
slot gacor
Kitila ahimiza uwekezaji Afrika Mashariki | Nipashe

Kitila ahimiza uwekezaji Afrika Mashariki

By Faustine Feliciane , Nipashe
Published at 02:02 PM Jan 27 2026
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo katikati akizungumzia Kongamano hilo limeandaliwa kwa pamoja na Taasisi ya Eastern Africa Association (EAA) na FTI Consulting.
Picha: Mpigapicha Wetu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo katikati akizungumzia Kongamano hilo limeandaliwa kwa pamoja na Taasisi ya Eastern Africa Association (EAA) na FTI Consulting.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, amefungua Kongamano la Uwekezaji la East Africa Prospect 2026 jijini London, Uingereza na kuhamasisha uwekezaji nchini na katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Kongamano hilo limeandaliwa kwa pamoja na Taasisi ya Eastern Africa Association (EAA) na FTI Consulting, likiwakutanisha mabalozi, viongozi wa taasisi za uwekezaji na sekta binafsi kujadili mwelekeo wa kisiasa na kiuchumi wa ukanda huo kwa mwaka 2026 na kuendelea.

Katika hotuba yake, Profesa Mkumbo amesisitiza umuhimu wa nchi za Afrika Mashariki kuimarisha ushirikiano wa kikanda katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo, hususan sekta za miundombinu, nishati na anga, akieleza kuwa miradi ya pamoja ni nguzo ya kuvutia uwekezaji wa muda mrefu na kukuza maendeleo jumuishi.

Aidha, ameeleza miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Tanzania ikiwemo Reli ya Kisasa (SGR) na Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), akisema miradi hiyo inaongeza muunganisho wa kikanda, inapunguza gharama za usafirishaji na kufungua fursa za biashara na ajira.

Prof. Mkumbo amewahakikishia wawekezaji kuwa Tanzania inaendelea kuwa nchi salama, thabiti kisiasa na yenye sera zinazotabirika, huku akitoa wito kwa nchi za Afrika Mashariki kuendeleza mshikamano wa kikanda kama njia ya kukuza uchumi na ustawi wa wananchi.