slot gacor
slot gacor
slot gacor
Njombe yapanda miti kuhifadhi vyanzo | Nipashe

Njombe yapanda miti kuhifadhi vyanzo

By Elizabeth John , Nipashe
Published at 07:22 PM Jan 27 2026
Njombe yapanda miti  kuhifadhi vyanzo
Picha:Mpigapicha Wetu
Njombe yapanda miti kuhifadhi vyanzo

Serikali ya Mkoa wa Njombe imeadhimisha siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa zoezi kubwa la kupanda miti elfu 20,000 katika vyanzo vya maji vya Kibena Howard na Ijunilo. Hatua hii inalenga kulinda na kuhifadhi vyanzo muhimu vya maji katika mkoa huo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Juma Sweda, amesema mkakati huu ni sehemu ya juhudi za kurejesha na kulinda uoto wa asili wa mkoa huo. Aidha, amewaonya wananchi kuacha vitendo vinavyosababisha moto, kwani moto husababisha hasara kubwa kwa wakulima na mazingira kwa ujumla.

Kwa upande wake, Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Njombe (NJUWASA), Mhandisi Robert Lupoja, amebainisha kuwa jumla ya miti 20,000 imepandwa katika siku hiyo, huku mpango mzima ukilenga kupanda miti elfu 80,000 katika maeneo mbalimbali ya vyanzo vya maji mkoani Njombe.

Zoezi hilo limehudhuriwa pia na wadau mbalimbali wa mazingira, wakiwemo wawakilishi wa Mamlaka ya Bonde la Mto Rufiji na timu ya maofisa kutoka Benki ya CRDB. Kwa niaba ya benki hiyo, Kaimu Meneja wa Tawi la Njombe, John Nchimbi, ameahidi kuendelea kushirikiana na wananchi katika juhudi za kulinda vyanzo vya maji kupitia huduma ya Takati DP, ambayo inalenga kuhifadhi mazingira kwa ajili ya vizazi vijavyo.