slot gacor
slot gacor
slot gacor
NSSF yashinda Wiki ya Fedha | Nipashe

NSSF yashinda Wiki ya Fedha

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 12:34 PM Jan 28 2026
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Balozi Dk. Batilda Burian.
Picha: Mpigapicha Wetu
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Balozi Dk. Batilda Burian.

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeibuka mshindi wa kwanza katika kundi la watoa huduma za hifadhi ya jamii wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yaliyofanyika jijini Tanga. Ushindi huo umetokana na mchango na ushiriki wake madhubuti katika utoaji wa huduma na elimu ya kifedha kwa wananchi.

Tuzo hiyo ilikabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Balozi Dk. Batilda Burian, kwa Meneja wa NSSF Mkoa wa Tanga, Nuhu Mbaga, katika hafla ya kufunga maadhimisho hayo.

Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yaliandaliwa na Serikali kupitia Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na wizara za kisekta, ikiwemo Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano ya Kazi, pamoja na taasisi zilizo chini ya wizara hiyo, ikiwemo NSSF.

Kupitia ushiriki wake katika maadhimisho hayo, NSSF iliendelea kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa wananchi, kuandikisha wanachama wapya, pamoja na kuhamasisha wanachama waliopo kutumia mifumo ya kidijitali katika kupata huduma mbalimbali.

Mifumo iliyotumika ni pamoja na NSSF Portal, NSSF App na huduma ya USSD (15200#), inayowawezesha wanachama kupata taarifa za michango yao, kutengeneza namba za kumbukumbu za malipo (Control Number), kulipia michango, pamoja na kufungua madai ya mafao kwa njia ya mtandao.Maadhimisho hayo yamehitimishwa rasmi Januari 26, 2026, katika Viwanja vya Usagara, jijini Tanga.