slot gacor
slot gacor
slot gacor
Serikali: Ifikapo 2023 asilimia 80 ya Watanzania kupata elimu ya fedha | Nipashe

Serikali: Ifikapo 2023 asilimia 80 ya Watanzania kupata elimu ya fedha

By Hamida Kamchalla , Nipashe
Published at 10:16 AM Jan 19 2026
 Kaimu Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Dionisia Mjema.
Picha: Mpigapicha Wetu
Kaimu Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Dionisia Mjema.

Serikali kupitia Wizara ya Fedha inaendelea kutekeleza mkakati maalum wa kuwalinda watumiaji wa huduma za fedha kwa kuwapatia elimu ya fedha, ikiwa ni jitihada za kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2030, angalau asilimia 80 ya Watanzania wawe wamepata uelewa wa elimu hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Dionisia Mjema, wakati wa maandalizi ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara, jijini Tanga.

Mjema amesema kuwa katika maadhimisho hayo, elimu mbalimbali kuhusu huduma za fedha zitatolewa kwa wananchi, lengo likiwa ni kuongeza uelewa wa watumiaji wa huduma hizo nchini, kufuatia matokeo ya utafiti uliofanywa na Wizara ya Fedha.

Ameeleza kuwa Wizara imefanya tafiti za upatikanaji wa huduma za fedha katika vipindi tofauti kuanzia mwaka 2006, 2013, 2017 hadi 2023, ambapo imebainika kuwa ni asilimia 53.5 tu ya wananchi wanaotumia huduma za fedha.

Amesema kuwa kati ya hao, wengi wanapata huduma kupitia benki za biashara, bima na makampuni ya simu, hata hivyo utafiti umeonesha kuwa wananchi wengi bado hawana uelewa wa kutosha kuhusu huduma rasmi za fedha.

“Katika utafiti wetu, tulipokutana na wananchi, ilibainika kuwa wengi wanatumia huduma za fedha bila kufahamu kikamilifu huduma rasmi zilizopo,” amesema Mjema.

Kutokana na hali hiyo, amesema Wizara imeweka mkakati wa kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2030, angalau asilimia 80 ya wananchi wawe wamepata elimu ya fedha, akisisitiza kuwa elimu hiyo itawezesha wananchi kufanya maamuzi sahihi ya kifedha na kuboresha uchumi wao.

“Ni imani yetu kwamba baada ya elimu hii, wananchi wa Tanga na maeneo mengine wataboresha uchumi wao na kunufaika zaidi na huduma rasmi za fedha,” amesisitiza Mjema.