slot gacor
slot gacor
slot gacor
Uhaba wa malighafi wakwamisha viwanda Singida | Nipashe

Uhaba wa malighafi wakwamisha viwanda Singida

By Thobias Mwanakatwe , Nipashe
Published at 03:44 PM Jan 23 2026
Uhaba wa malighafi wakwamisha viwanda Singida
Picha:Mpigapicha Wetu
Uhaba wa malighafi wakwamisha viwanda Singida

Mkoa wa Singida umetajwa kuwa na fursa kubwa ya kukuza uchumi wa viwanda na kuchangia kwa kiasi kikubwa pato la taifa, hata hivyo juhudi hizo bado zinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa malighafi unaosababisha baadhi ya viwanda kusimamisha uzalishaji kila mwaka.

Kauli hiyo imetolewa leo na Brigedia Jenerali Charles Ndiege wakati wa ziara ya mafunzo kwa vitendo ya washiriki wa Kozi ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) waliotembelea viwanda mbalimbali mkoani Singida, ikiwa ni sehemu ya kujifunza utekelezaji wa sera na mipango ya maendeleo katika mazingira halisi.

Brigedia Ndiege amesema changamoto kubwa inayovikabili viwanda vingi ni kushindwa kufanya kazi kwa msimu mzima kutokana na utegemezi wa malighafi zinazotokana na kilimo cha mvua, hali inayosababisha uzalishaji kuwa wa msimu na usio na uhakika.

Amefafanua kuwa hali hiyo huathiri mnyororo mzima wa maendeleo ya kiuchumi, kuanzia kwa mkulima anayekosa soko la uhakika, hadi kwa mfanyakazi wa kiwandani anayepoteza ajira au kipato kutokana na viwanda kusimama.

“Viwanda vinaposimama au kupunguza uzalishaji, ajira hupungua, mapato ya wananchi hushuka na mchango wa sekta ya viwanda katika pato la taifa hudhoofika,” amesema Brigedia Ndiege.

1