Vijana wametakiwa kutumia mitandao ya kijamii vizuri ili waweze kujikwamua kiuchumi kutokana na fursa zinazopatikana mtandaoni ikiwamo za kibiashara.
Aidha imesisitizwa wanapaswa kuoina intaneti kama nyenzo muhimu ya kujipatia kipato na kwamba dunia ya sasa inahitaji ubunifu na matumizi sahihi ya teknolojia.
Ushauri huo umetolewa leo Januari 21 na Mwigizaji Idriss Sultan alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu fursa na namna vijana wanavyoweza kunufaika na mitandao ya kijamii.
“Tayari sasa hivi kila kitu unachokiona kipo mtandaoni hivyo Intaneti siyo kwa ajili ya burudani pekee. Ni soko kubwa sana. Ukiitumia vizuri, unaweza kupata wateja kutoka sehemu yoyote bila hata kuwa na duka” amesema Idriss ambaye pia ni Balozi wa Mtandoa wa Halotel
Amesema mtandao huo umeendelea kuthibitisha dhamira yake ya kutoa huduma bora na za kisasa kwa wateja wake nchini, baada ya kuzindua rasmi huduma mpya ya intaneti.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kutoka kampuni hiyo, Roxana Kadio, amesema wanatambua mahitaji ya wateja katika matumizi ya intaneti ya uhakika na yenye kasi, jambo lililoifanya kuwekeza kwa kiwango kikubwa katika miundombinu ya teknolojia ya 5G.
“...Imejidhatiti kuhakikisha wateja wake wanapata huduma bora, za uhakika na zinazoendana na kasi ya maendeleo ya teknolojia duniani hivyo huduma hiyo ni sehemu ya mkakati wetu wa muda mrefu wa kuboresha mawasiliano na kuchochea maendeleo ya kidijitali nchini” amesema
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED