slot gacor
slot gacor
slot gacor
'Iran haitaanza uchokozi, lakini iko tayari kwa vita ikishambuliwa’ | Nipashe

'Iran haitaanza uchokozi, lakini iko tayari kwa vita ikishambuliwa’

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 02:48 PM Jan 12 2026
Abbas Araghchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran
Picha: Mtandao
Abbas Araghchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, amesema Tehran haina mpango wa kuchukua hatua za kijeshi, lakini iko tayari kwa vita ikishambuliwa.

Akiwahutubia mabalozi wa kigeni mjini Tehran, Abbas Araghchi alisema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitaki vita, huku akiwaonya wapinzani dhidi ya mpango mbaya wowote.

Anasema Iran imejiandaa zaidi kuliko wakati wa mzozo wake wa siku 12 na Israel mwezi Juni, mwaka uliopita.

Araghchi pia imetetea hatua ya udhibiti mtandao wa itaneti unaendelea katikati ya machafuko akiongeza kuwa hatua hiyo iitadumishwa hadi pale tutakapojiridhisha kuwa hakuna vitisho tena.

Waziri wa mambo ya nje, anasema machafuko ya hivi majuzi yamebadilika kutoka kwa maandamano hadi kwa kile anachotaja kama operesheni za kigaidi, akirejelea kaulirasmi uliotolewa na vyombo vya habari vya Iran na vyombo vya usalama wiki iliyopita.

Aidha amesema Iran iko tayari kwa mazungumzo, lakini kwa kile anachoeleza kuwa haki, heshima na masharti sawa - akisisitiza msimamo wa Tehran juu ya mazungumzo na Washington tangu mzozo wa Juni.

Chanzo: BBC