Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) limeonya kuwa inayoshikilia mpini na kuamua hatima ya vita vyovyote vitakavyoanzishwa na Marekani.
Alisema kama Marekani itaishambulia Iran, nguvu itakayotumika itaishangaza dunia na haitatajiwa kama inatoka ndani ya taifa hilo.
Msemaji wa IRGC, Brigedia Jenerali Ali-Mohammad Naeini, alisema siku ya Jumatano, kwamba shinikizo la kijeshi lilalofanywa na Marekani hakutazaa matunda.
Ofisa huyo wa jeshi, alisema majaribio ya kuitisha Iran kupitia ishara na utumaji wa ndege za kivita, pamoja na meli ya kubeba ndege ya Marekani jirani na Iran, sio jambo jipya kwani mbinu hiyo ni ya zamani inayotumiwa na Marekani.
Kwa mujibu wa kamanda huyo, kushindwa kwa haraka nguvu uasi unaoungwa mkono na Marekani nchini Iran, maofisa wa Marekani wamejaribu kuchochea mvutano na kueneza hofu ndani ya jamii ya Iran.
Wakati huo huo, Msemaji wa serikali ya Iran ameonya kwamba, jeshi la nchi hiiyo litajibu mapigo ili kutetea mamlaka ya kujitawala na uhuru wa taifa hilo.
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED