slot gacor
slot gacor
slot gacor
Rwanda yaishtaki London kwa kukiuka makubaliano | Nipashe

Rwanda yaishtaki London kwa kukiuka makubaliano

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 04:37 PM Jan 29 2026
news
Picha Mtandao
Rwanda yaishtaki London kwa kukiuka makubaliano

TAIFA la Rwanda limeanzisha kesi mbele ya Mahakama ya Kudumu ya Usuluhishi huko Hague, ikidai ukiukaji wa makubaliano ya uhamiaji ya mwaka 2022 na London.

Mkataba huo wenye utata unaelezea kurejeshwa kwa wahamiaji waliofika kinyume cha sheria nchini Uingereza. Na kwamba mkataba huo ulitupiliwa mbali mwaka 2024 na serikali mpya ya Labour iliyochaguliwa.

Taarifa ya Rwanda iliyotolewa leo inadai kwamba Uingereza ilikiuka makubaliano kati ya nchi hizo mbili kuhusu baadhi ya masharti ya kifedha.

Ingawa mradi huo ulitupiliwa mbali hadharani Julai 2024 na mamlaka ya Uingereza, kulingana na Kigali, majadiliano hayakufikia makubaliano mwaka huo, si kwa masharti ya kuvunja rasmi makubaliano wala kwa kuachana na malipo mawili yaliyopaswa kutekelezwa mwaka 2025 na 2026, kila moja ikiwa na jumla ya pauni milioni 50.

Mnamo mwezi Machi mwaka jana, Rwanda ilidai malipo ya deni lililobaki la makubaliano ya uhamiaji, wiki moja tu baada ya kutangazwa kwa kusitishwa kwa misaada mingi ya kifedha ya Uingereza. Vikwazo hivyo vilihusishwa na mzozo mashariki mwa DRC.

Uingereza “imeweka wazi kwamba haina nia ya kufanya malipo yoyote zaidi chini ya mkataba,” Kigali ilisema wiki hii, ikiongeza kuwa nchi hiyo pia imeshindwa kuheshimu ahadi yake ya kuwapa makazi wakimbizi walio hatarini wanaopewa hifadhi na Rwanda.

“Tutatetea kwa nguvu msimamo wetu ili kuwalinda walipa kodi wa Uingereza,” msemaji wa Waziri Mkuu wa Uingereza alijibu.

RFI