Mkutano wa Pili wa Bunge la 13 umeanza leo, Januari 27, 2026, jijini Dodoma, ambapo wabunge watajadili mwelekeo wa Serikali , mipango ya maendeleo na utekelezaji wa majukumu ya kibunge.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Elimu kwa Umma cha Ofisi ya Bunge, mkutano huo utaendelea hadi Ijumaa, Februari 6, 2026, na utahusisha shughuli mbalimbali ikiweno kiapo cha uaminifu kwa wabunge wateule ambao hawakupata fursa ya kuapishw akwenye mkutano w akwanza wa bunge hilo.
Katika mkutano huo, kutakuwa pia na kipindi cha maswali ya Bunge ambapo jumla ya maswali 160 yanatarajiwa kuulizwa na kujibiwa na Mawaziri wa sekta mbalimbali.
Aidha, siku ya Alhamisi kutakuwa na kipindi cha Maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu, ambapo takriban maswali 16 yataulizwa na wabunge na itakua mara ya kwanza kwa waziri Mkuu Mwigulu Nchemba kuulizwa maswali ya papokwa papo toka ateuliwe na Rais Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa huo.
Vilevile, Wabunge wanatarajiwa kujadili hoja za Serikali kupitia mjadala wa Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan aliyoitoa bungeni Novemba 13 wakati wa ufunguzi wa Bunge la Kumi na Tatu.
Hotuba hiyo inaeleza mwelekeo na vipaumbele vya Serikali kwa kipindi kijacho.
Bunge pia litakaa kama Kamati ya Mipango kujadili mpango elekezi wa maendeleo wa uda mrefu wa miaka 25,mpango wa kwanza wa Maendeleo ya Taifa wa miaka mitano pamojana mapendekezo ya Mpango wa maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2026.2027
Mbali na hayo, mkutano huo utahusisha uchaguzi wa Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge pamoja na wawakilishi wa vyama mbalimbali vya kibunge, ikiwa ni sehemu ya majukumu ya kikatiba ya Bunge.
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED