slot gacor
slot gacor
slot gacor
Vijana wanakwama hapa kufikia malengo | Nipashe

Vijana wanakwama hapa kufikia malengo

By Halfani Chusi , Nipashe
Published at 10:19 PM Jan 29 2026
vijana wakipata mafunzo
PICHA: Halfan Chusi
vijana wakipata mafunzo

Kukosekana kwa elimu ya afya uzazi kwa vijana kumetajwa ni miongoni mwa sababu zinazo wafanya washindwe kufikia ndoto zao.

 Hayo yamesemwa jana Mkoani Dar es Salaam na Mkufunzi wa Kitaifa Masuala ya Afya ya Uzazi kwa Vijana kutoka Wizara ya Afya Dk. Zuhura Majafa alipokuwa akiwajengea vijana uelewa kuhusu masuala hayo.

 Dk. Zuhura alisema kazi yao ni kutengeneza sera sheria na miongozo kuhusu afya ya uzazi kwa vijana ili zisaidie upatikanaji wa huduma rafiki kwao.

 Alisema kazi nyingine ni kuwafundisha umuhimu wa kuwekeza kwaajili ya afya ya uzazi akisisitiza kwamba asilimia 60 ya watanzania ni vijana hivyo kuna kila sababu ya kutunza afya zao ili kutopoteza nguvu kazi ya taifa.

 “Tukimaliza hilo tunakwenda kuwafundisha watoa huduma kwa vijana. Vyuoni mmonyoko wa maadili umekuwa mkubwa ikiwamo mimba za utotoni wengi wao hawafikii ndoto zao kwa sababu wameshindwa kuhimili mihemko ya ujana ndio maana leo tupo hapa kuwalinda ili wavuke salama katika daraja la ujana” alisema 

 Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Hainece Francis miongoni mwa waliopokea mafunzo hayo alisema janga la uzazi na ukatili wa kijinsia linawakumba vijana wengi kwa sababu hawajui kitu cha kufanya wanapokutana na mazingira hayo.

 “Kwa sasa kumekuwa na wimbi la kusambaza picha za utupu mitandaoni ninafikiri inatokea hivyo kwa sababu vijana wengi hawajui matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii.

 “Vijana wanapaswa kujua namna sahihi ya kutumia uzazi wa mpango wanavyopata hizi semina wanajua vitu vingi serikali igawe kondomu kwa vijana ili waweze kujikinga na magonjwa ya zinaa” alisema Hainece  

1
Naibu Waziri wa Afya na Migahawa wa Chuo Kikuu Shirikishi cha Elimu Dar es Salaam (DUSE) Joctan Musa alisema mafunzo hayo ni muhimu kwa kuwa wamejifunza kuhusu masula ya lishe, afya ya uzazi na kwamba vitu vingi kwake vilikuwa ni vigeni. 

 Alisema kupitia mafunzo hayo yaliyotolewa kwa hisani ya mradi wa AHADI unaofadhiliwa na Word Vision Tanzania na kutekelezwa na KIWOHEDE amejua namna ya kutumia afya yake na vyakula vya kujenga mwili sambamba na madhara ya kuegemea upande mmoja wa jinsia.

 “Mimi hata nikienda kijijini nitawaeleza umuhimu wa kuwa na usawa wa kijinsia na haki zipi mtoto hatakiwi kunyimwa ikiwamo elimu nimejifunza vitu vingi, ambavyo vitaenda kunisaidia zaidi na kuelimisha jamii nikipata nafasi ya kuwashauri walioko mtaani nitawaambia afya ni mtaji. 

 “Nitawashauri kuna vitu ambavyo sio vya kufanya na kuithamini afya yao kuanzia kwenye chakula, shughuli za kijamii, kufanya mazoezi nitawashauri wajiingize katika mambo yanayowaweka katika nafasi nzuri kwenye maisha yao. 

 Vilevile aliishuku serikali kwa kuanzisha Wizara ya Vijana inayoleta chachu na inawapa nafasi ya kujua hulka zao na kueleza Vikwazo wanavyokutana navyo kwa sababu wanakuwa na uwanja mpana wa kuelezea.