Jumla ya wasichana 83,000 kutoka kwenye mazingira magumu katika mikoa 10 ya Tanzania wamenufaika na kupata misaada mbalimbali ya ujasiliamali kupitia shirika lisilo la kiserikali linajihusisha na kusaidia watoto wa kike wanaotoka kwenye mazingira magumu na familia duni hapa nchini (CAMFED).
Mkurugenzi Mtendaji wa CAMFED Anna Sawaki amesema hayo leo wakati akizungumzia mafanikio ya wasichana hao wakati akifunga mkutano Mkuu wa mwaka 2025 uliofanyika mkoani hapa.
Anasema kwa kushirikiana na serikali wamejipanga kuhakikisha vijana wanapata baadhi ya wadau wa kuwasaidia vitendea kazi mbalimbali ili waweze kukuza biashara zao.
Hata hivyo Sawaki anasema wasichana hao bado wanauhitaji wa kusaidia katika.kukuza mifumo ya biashara, masoko na kuongezewa thamani kwa wale wanaofanya biashara ya kilimo hasa wanaolima kilimo cha kisasa ambao wameibuka kibiashara na kutamani kwenda kuuza nje ya nchi.
Hivyo amewataka wasichana hao kuamka na kutumia usichana wao katika kujiletea maendeleo huku wakijiamini na kuthamini kazi zao kabla ya wengine hawajatambua umuhimu wao.
Mwenyekiti wa Mtandao wa wasichana wafadhiliwq wa CAMFED (CAMA) Taifa Shamsa Mkurungo amesema wamefanikiwa kusaidia watoro 114,000 na kurudisha wanafunzi walioacha shule.
Pia anasema wamepata mikopo 511 isiyokuwa na riba kutoka CAMFED iliyoweza kusaidia kukuza biashara zao samnamba na kupata mitaji ya kuanzisha biashara iliyosaidia ongezeko kubwa la wana CAMA katika kuanzisha biashara mwaka 2025.
Mmoja wa wanufaika wa CAMA kutoka Wilaya ya Kilosa mkoani hapa Mzizi Mtambwa ameishukuru CAMFED kwa kuanzisha programu hiyo iliyonsaidia kupata mafunzo mbalimbali ikiwemo ya uongozi na uchumi baada ya kumuokoa kutoka kwenye sintofahanu ya kumaliza kidato cha nne baada ya kukosa wa kumsomesha.
Anasema kupitia misaada ya CAMA ameweza kuendeleza kilimo cha mpunga kwa umwagiliaji na kuinua kutoka kuwa na uhakika wa 1000 hadi kufikia kuwa na uhakika wa 10,000 ya kulimia na kuajiri baadhi ya vijana na kupunguza ukosefu wa ajira.
Elina Lukindo ni mmoja wa wasichana waliosaidiwa na CAMFED anasema dhana ya kujiamini aliyofundishwa na CAMA imemsaidia kupata nafasi ya udiwani viti maalum Kata ya Gairo Wilayani Gairo mkoani hapa.
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED