slot gacor
slot gacor
slot gacor
Watakiwa kukabili unyanyapaa, ubaguzi dhidi watoa huduma VVU | Nipashe

Watakiwa kukabili unyanyapaa, ubaguzi dhidi watoa huduma VVU

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:39 PM Jan 29 2026
Washiriki wa mafunzo hayo
Picha: MNH
Washiriki wa mafunzo hayo

Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUCOHAS), kwa kushirikiana Wizara ya Afya na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS), zinaendelea kutekeleza mradi wa Afua Jumuishi;

Unaolenga kuondoa unyanyapaa na ubaguzi, miongoni mwa watoa huduma za afya kwa wagonjwa wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU) pamoja na watumiaji wa dawa za kulevya. 

Kikao cha siku tano kinafanyika mkoani Morogoro, kikilenga kuandaa nyenzo za  kufundishia, ili kuwajengea uwezo walimu  na wanafunzi wa vyuo vya kati, juu ya unyanyapaa na ubaguzi.

Akizungumza kuhusu utekelezaji wa mradi huo, Mkuu wa Chuo cha MUCOHAS, Dk. Bonny Betson, amesema mradi huo umejikita katika kuboresha uelewa, mitazamo na ujuzi wa watoa huduma. ili kuhakikisha huduma za afya zinazotolewa ni jumuishi, rafiki na zenye kuzingatia utu wa kila mteja.

“Huu ni mwaka wa tatu tangu tulipoanza mradi huu, na kwa sasa tumetekeleza awamu ya kwanza hapa MUCOHAS kwa wanafunzi na walimu, baada ya hapo tunapitia mtaala mdogo tulioutengeneza mahsusi kwa ajili ya kuendesha mafunzo haya,” amesema Dk. Betson.

Washiriki wa mafunzo hayo
Ameongeza kuwa kabla ya kuandaa mtaala huo, utafiti wa awali ulifanyika kwa wanafunzi na walimu waliopata mafunzo ili kubaini mahitaji halisi na changamoto zilizopo katika utoaji wa huduma na matokeo ya utafiti huo.

Anasema matokeo yalitumika kutengeneza mtaala unaolenga kutumika pia katika vyuo vingine vya afya nchini, ikiwa ni hatua muhimu ya kupunguza unyanyapaa na ubaguzi miongoni mwa watoa huduma za afya.

Utekelezaji wa mradi wa Afua Jumuishi unaendana na malengo ya serikali kupitia Wizara ya Afya, kuboresha huduma za afya kwa wananchi, hususan katika kuondoa unyanyapaa unaodhorotesha upatikanaji  na utumiaji wa huduma kwa watu wanaoishi na VVU Pamoja na watumiaji wa madawa ya kulevya. 

Mikakati iliyowekwa ili kutokomeza maambukizi ya VVU ifikapo mwaka 2030, kwa kuimarisha utoaji wa huduma rafiki, jumuishi na zenye usawa kwa wote.