slot gacor
slot gacor
slot gacor
NLD yatia mguu ubunge Peramiho | Nipashe

NLD yatia mguu ubunge Peramiho

By Thobias Mwanakatwe , Nipashe
Published at 05:44 PM Jan 29 2026
NLD yatia mguu ubunge Peramiho
PICHA: MPIGAPICHA WETU
NLD yatia mguu ubunge Peramiho

Mgombea wa ubunge katika jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma kupitia Chama cha NLD, Hamis Mhagama, amechukua fomu katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kuomba kuteuliwa kuwania nafasi hiyo.

Akizungumza leo, Januari 29, 2026, mara baada ya kukabidhiwa fomu na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Mhagama alisema endapo akifanikwa kuteulia na  kushinda kuwa mbunge, ataendeleza kilimo cha umwagiliaji pamoja na uchimbaji wa madini kama nguzo muhimu za kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa Peramiho.

Katibu Mkuu wa Chama cha NLD, Doyo Hassan Doyo, aliyemsindikiza mgombea huyo katika ofisi za INEC, alisema umefika wakati kwa wananchi wa Peramiho kufanya mabadiliko kwa kuchagua mbunge kutoka chama cha NLD, akidai kuwa uongozi uliopita kwa miaka mingi umeshindwa kuleta maendeleo ya maana katika jimbo hilo. 

Hadi leo wagombea wa  vyama vingine ambao tayari wamechukua fomu INEC kugombea jimbo hilo ni Rai Yusuf(AAFP) Shani Zinduka (SAU), Mohamed Hanifa ( UMD), Beatrice Muya (UPDP),Pili Dastan (CCK), Morice Nkongo(TLP), Mtemi Pachoto  (UDP) na Abdallah Ngonyani wa chama cha MAKINI.

Uchaguzi mdogo wa jimbo la Peramiho unafanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Jenista Mhagama, aliyefariki dunia mwishoni mwa mwaka jana.