slot gacor
slot gacor
slot gacor
Mashabiki wa Esperance wasafiri na SGR kutalii Moro | Nipashe

Mashabiki wa Esperance wasafiri na SGR kutalii Moro

By Christina Haule , Nipashe
Published at 01:54 PM Jan 30 2026
Klabu ya Esperance De Tunis.

Reli ya Kisasa ya Standard Gauge Railway (SGR) imeendelea kuthibitisha mchango wake katika kurahisisha usafiri na kukuza sekta ya utalii nchini, huku ikitoa huduma kwa Watanzania na wageni kutoka mataifa mbalimbali.

Hivi karibuni, baadhi ya mashabiki wa klabu ya Esperance De Tunis kutoka Tunisia wameonekana katika Stesheni ya SGR Magufuli jijini Dar es Salaam wakisafiri kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi mkoani Morogoro kwa shughuli za utalii. Tukio hilo linaakisi namna SGR inavyochochea utalii wa ndani na wa kimataifa.

Hatua hiyo pia inaonesha jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha miundombinu ya kisasa, hususan SGR, kama mkakati wa kukuza uchumi, biashara na kurahisisha usafirishaji wa abiria, mizigo na watalii.

Mashabiki hao wamechukua fursa ya uwepo wao nchini kutembelea vivutio vya utalii, huku wakisubiri mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Esperance De Tunis na Simba SC utakaochezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mamlaka za usafiri, SGR imekuwa zaidi ya reli ya abiria na mizigo, kwani imechangia kuongeza mzunguko wa biashara, kurahisisha usafiri kati ya mikoa na kuwa kichocheo muhimu cha ukuaji wa sekta ya utalii nchini.