slot gacor
slot gacor
slot gacor

Palmer hagusiki Chelsea | Nipashe


Palmer hagusiki Chelsea

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 12:46 PM Jan 29 2026
news
Picha Mtandao

Palmer hagusiki Chelsea

CHELSEA inamwona Cole Palmer kama "asiyegusika" huku kukiwa na taarifa za kuhusishwa na kutakiwa Manchester United.

Palmer ana mkataba na Chelsea hadi mwaka 2033 na anaonekana kama mchezaji muhimu katika mustakabali wa klabu hiyo.

Ripoti za hivi karibuni zimedokeza kwamba mchezaji huyo wa kimataifa wa England alikuwa akihisi kutokuwa na utulivu jijini London na alikuwa tayari kuhamia Man United ili arudi kaskazini magharibi, lakini Chelsea wanaamini mchezaji huyo anafuraha hapo Stamford Bridge kama vile kocha mkuu, Liam Rosenior.

Kocha Rosenior alipoulizwa na ESPN kama Palmer ana furaha klabuni hapo, alijibu: "Ndiyo na ndiyo. 

"Cole ni mchezaji wa ajabu. Sishangai kuhusu uvumi wake. Cole yuko hapa, anafurahi sana.

"Cole anafurahi sana. Tumekuwa na mazungumzo mengi naye kuhusu jinsi tunavyoweza kuifanya timu hii iwe bora zaidi, jinsi anavyoweza kuimarika na jinsi ninavyoweza kumsaidia  kwa sababu anapenda kuwa hapa na anataka kuwa mchezaji wa Chelsea.

"Huwezi kuzuia uvumi, lakini uvumi fulani uko mbali sana na ukweli, hakuna haja ya kujadiliana kuhusu hilo."

Msimu huu Palmer ameathiriwa na majeraha na pia ilimfanya akose mechi ya ushindi ya Jumapili dhidi ya Crystal Palace.

Palmer alijiunga na Chelsea kutoka Manchester City kwa ada ya pauni milioni 40 mwaka 2023 na amefunga mabao 41 na kutoa pasi za mabao 20 katika mechi zake 81 za ligi Kuu kwa Blues hao.