slot gacor
slot gacor
slot gacor
Sadio Mane, Pape Thiaw nani shujaa wa Senegal? | Nipashe

Sadio Mane, Pape Thiaw nani shujaa wa Senegal?

By Halfani Chusi , Nipashe
Published at 02:50 PM Jan 20 2026
 Sadio Mane.
Picha: Mtandao
Sadio Mane.

Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) zimetamatika kwa taifa la Senegal kuibuka mshindi kwa kuibwaga mwenyeji, Morocco kwa mabao 1-0.

Mjadala uliobaki masikioni na machoni mwa wapenda mpira Afrika na duniani ni nani anayepaswa kuwa shujaa wa michezo huo ambao licha ya kutoa bingwa lakini ulikumbwa na vurugu.

Je? ni Sadio Mane au kocha wake Pape Thiaw ambaye anapaswa kupewa pongezi, huku mmoja akihamasisha wenzake kurejea uwanjani baada ya kutokea vurugu na mwingine akihamasisha wachezaji kuondoka uwanjani.

Tukio kuu katika fainali hiyo litakalosalia katika kumbukumbu ya historia ya michuano hiyo ni katika dakika ya 98 pale Senegal walipotoka uwanjani na kususia mechi hiyo kwa muda wa dakika 17.

Chanzo kikiwa ni uamuzi wa refa Jacques Ndala aliyewapa Morocco penalti baada ya kutumia uamuzi wa VAR. Malick Diouf wa Senegal alidaiwa kumchezea rafu mshambulaiji wa Morocco, Brahim Diaz.

Hatua hiyo ilimlazimu kocha wa Senegal Pape Thiew kuwahamasisha wachezaji wake kutoka kabisa uwanjani akilalamika kuwa wamedhulumiwa.

Mchezaji aliyebaki uwanjani ni Sadio Mane tu, nahodha wa Senegal aliyewashauri wenzake kurejea, na baada ya dakika 17 walirejea na kukubali kuendelea na mchezo.

Kwa bahati nzuri kwa Senegal, Brahim Diaz aliyefunga mabao matano kwenye michuano hiyo, aliipiga penalti hiyo iliyonyakwa na kipa Eduad Mendy wa Senegal. 

Baada ya kutamatika ziliongezwa dakika za ziada 30 ndipo Senegal ikaibuka mshindi kwa bao 1-0 lililofungwa na nyota wao Pape Gueye na kuwafanya kunyakua kombe hilo.

Je? kati ya wawili hao nani anapaswa kupewa pongezi, kocha aliyehamasisha wachezi kuondoka uwanjani ambapo walitii amri hiyo na baadaye Sadio Mane kuwafuata na kuwahamasisha kurudi na kuendelea na mchezo ambao baadaye waliibuka na ushindi.