Wabunge pamoja na mashabiki wa klabu za Yanga na Simba wanatarajiwa kushiriki zoezi la kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wenye uhitaji, katika bonanza la Bunge litakalofanyika Januari 31, jijini Dodoma.
Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi, litaambatana na michezo na burudani mbalimbali, ikiwemo kukimbiza kuku, mbio, mpira wa pete, kuvuta kamba, mpira wa kikapu pamoja na kushindana ya kula.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Bunge Bonanza ambaye pia ni Mbunge wa Makete, Festo Sanga, amesema tamasha hilo litafanyika katika uwanja wa John Merlini Mipango jijini Dodoma.
Amesema mashabiki wa Simba na Yanga wanatarajiwa kupimana nguvu katika bonanza hilo litakalowakutanisha wabunge, wafanyakazi wa Bunge, wizara pamoja na taasisi mbalimbali.
“Bonanza hili ni maono ya Bunge, menejimenti na Spika kuhakikisha linakuwa kiungo cha kuimarisha mahusiano na wadau mbalimbali, kwa kuwa Bunge ni chombo cha wananchi,” amesema Sanga.
Ameongeza kuwa bonanza hilo pia linalenga kudumisha umoja na mshikamano kati ya Bunge na taasisi mbalimbali, sambamba na kuunga mkono sekta ya michezo.
© 2026 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED