slot gacor
slot gacor
slot gacor
Yanga yakosa uwanja wa nyumbani KMC Complex ikifungiwa | Nipashe

Yanga yakosa uwanja wa nyumbani KMC Complex ikifungiwa

By Adam Fungamwango , Nipashe
Published at 01:42 PM Jan 29 2026
news
Picha Mtandao
Yanga yakosa uwanja wa nyumbani KMC Complex ikifungiwa

KLABU ya Yanga italazimika kuhama Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam na kutafuta uwanja mwingine baada ya kufungiwa kutumiwa kwa kile kilichoelezwa ni kukosa vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu.

Yanga inautumia KMC Complex, uliopo Mwenge kama uwanja wake wa nyumbani, hivyo kufungiwa kwa uwanja huo kutailazimu kusaka uwanja mwingine kuutumia kwenye michezo yake ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF), jana lilitoa taarifa ya kuufungia uwanja huo mpaka pale utakapofanyiwa maboresho na baadaye kukaguliwa.

TFF imesema sababu ya kufungia uwanja huo ni miundombinu, bila ya kufafanua zaidi kwamba ni miundombinu ya aina gani.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na Cliford Mario Ndimbo, Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, imesema miundombinu ya uwanja huo haikidhi matakwa ya kikanuni kama iliyoainishwa kwenye masharti ya kanuni ya leseni za klabu.

Uwanja huo umefungiwa siku chache tu baada ya mchezo wa Ligi Kuu kati ya Yanga dhidi ya Dodoma Jiji uliopigwa, Jumanne iliyopita, Yanga ikishinda mabao 3-1.

Mechi hiyo ilichezwa usiku, ikiwa ni kwa mara ya pili mechi ya Ligi Kuu kuchezwa muda huo, wa kwanza ulikuwa kati ya Singida Black Stars dhidi ya JKT Tanzania uliochezwa Januari 20 mwaka huu, maafande wakishinda bao 1-0.