slot gacor
slot gacor
slot gacor
Zawadi anavyoipa zawadi Simba Queens msimu huu | Nipashe

Zawadi anavyoipa zawadi Simba Queens msimu huu

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 11:45 AM Jan 26 2026
news
Picha Mtandao
Zawadi anavyoipa zawadi Simba Queens msimu huu

STRAIKA Zawadi Usanese raia wa Rwanda, amekuwa mwokozi wa Simba Queens katika michezo mingi migumu ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayoendelea.

Zawadi, aliyesajiliwa msimu huu akitokea AS Kigali ya Rwanda, amefunga mabao matano mpaka sasa kwenye ligi katika michezo muhimu ambayo ilionekana kama isingeweza kupata ushindi au ingepoteza.

Uongozi wa Simba Queens kwenye Ligi Kuu mpaka sasa kwa kiasi kikubwa umechangiwa sana na mchezaji huyo ambapo kila mechi ilipoonekana kuwa ngumu, Zawadi ambaye mechi nyingi amekuwa akitokea benchi anakuwa mwokozi.

Alifunga bao pekee ugenini kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Ceasiaa Queens katika mchezo ambao ilionekana kama Simba Queens ingelazimishwa sare.

Alifunga tena bao pekee katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa, Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa dhidi ya Ruangwa Queens.

Ulionekana mchezo mgumu, lakini Zawadi aliyeingia kipindi cha pili alipachika bao lililoipa Simba Queens ushindi wa bao 1-0.

Katika mchezo dhidi ya JKT Queens ilionekana kama Simba Queens inakwenda kupoteza mchezo lakini dakika za mwisho straika huyo alisawazisha mechi ikaisha kwa bao 1-1.

Alifunga bao la ushindi katika mchezo dhidi ya Mashujaa FC, Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma, katika mchezo ulioonekana timu hizo zingekwenda sare ya bao 1-1.

Ijumaa iliyopita alifunga tena bao pekee katika mchezo ambao Simba Queens ilishinda bao 1-0 dhidi ya Alliance Girls.

Alilifunga dakika za mwisho akitokea benchi, huku mashabiki wengi wakiamini mchezo huo ungeisha kwa kwa sare.